BALOZI SEIF NA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA WAKUFUNZI WA SENSA
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd amesema mafanikio ya Sensa
ya mwaka 2012 yanategemea umakini wa Wakufunzi wa Sensa ambao wanajukumu
la kuhakikisha kuwa mafunzo waliyoyapata yanawafikia Makarani wa Sensa
ili kuiwezesha Sensa ya mwaka huu kuwa na mafanikio zaidi ya mwaka 2002.
Balozi
Seif ameyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya
Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa yaliyofanyika leo ukumbi wa Chuo Kikuu
cha Zanzibar Tunguu
Amesema
Wakufunzi hao wanajukumu kubwa la kuhakikisha Sensa ya mwaka 2012
inafanikiwa kwani wao ndio ambao wataenda kuwaelimisha makarani wa Sensa
yale ambayo yanahitajika na kufanyiwa kazi.
“Dhamana
ya mafanikio ya Sensa hii ipo mikononi mwenu,hivyo ni imani ya Serikali
kuwa mtatumia juhudi na maarifa ili lengo hilo liweze kufanikiwa na
kujenga imani kwa wananchi kwamba rasilimali zilizotumika zimeleta
mafanikio yaliyokusudiwa” Amesema Balozi
Amefahamisha
kuwa mafanikio ya Sensa yaliyopatikana mwaka 2002 yaliipa heshima kubwa
Zanzibar katika nyanja za kimataifa na kupelekea baadhi ya nchi za
Afrika ikiwemo Ghana, Angola,Sudani kuja kujifunza jinsi Zanzibar
ilivyofanya sensa hiyo kwa mafanikio makubwa.
Ameongeza
kuwa kutokana na matayarisho ambayo yamefanywa na Serikali ya Mapinduzi
kwa kushirikiana na Serikali ya Muungano anaamin kuwa Sensa ya mwaka
huu itakuwa na mafanikio zaidi ili iwe dira kwa nchi nyingine zaidi
duniani.
Aidha
amewataka Wakufunzi hao kuwatanabahisha makarani wa Sensa juu ya
changamoto ambazo wanaweza kukabiliana nazo na njia za kuziepuka wakati
wa zoezi la Sensa litakapoanza.
RAIS MPYA ZAMBIA AKARIBISHWA IKULU
Rais mpya wa Zambia bw Sata amekaribishwa Ikulu na kukabidhiwa rasmi mjengo na Rais wa zamani Banda. Hawa jamaa wamepiga hatua sana kidemokrasia.
Serikali mpya tayari imeanza kazi kwa kudhibiti matumizi mabaya ya mali za umma. Kwa mfano, kumbe chama tawala MMD kilikuwa kinatumia magari ya jeshi kwa kampeni. Magari hayo yamekamatwa yote.
MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI UGANDA ATIWA NDANI KWA UFISADI
HAPA JAMAA ANAPANDA GARI KWENDA SERO
Dr. Gilbert Bukenya alikuwa Makamu wa Rais asiye mwoga akijulikana kama "mahogany" ule mti mnene ambao unahimili vishindo, wiki hii katiwa ndani kwa ufisadi miezi michache baada ya Rais Museveni kumweka benchi.
Amenukuliwa akidai kkuwa haogopi kwenda jela.Ukiisoma hii utaona mtitiriko wa matukio ambayo yamemfikisha hapa alipo leo. Akiwa kama mtu mwenye nguvu nchini Uganda na Kigogo haswa, wengi wanajiuliza je ndio mwisho wake? hasa baada ya yeye kkuwahi kunukuliwa akisema kuwa serikali ya Uganda ilikuwa inatawaliwa na "MAFIA" fulani, hapa akimaanisha Museveni na watu wake. Tangu wakati huo kisiasa ameanza kuyumba hadi amefikia hatua ya kulala sero.
KAGAME ANAVYOWAZA JUU YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA NCHI YAKE
Rais Paul Kagame, ni kiongozi wa aina yake katika Bara la Afrika kwa sasa. Ni mtu ambaye hata nchi yetu Tanzania tunamhitaji sana kama kweli tunataka kuendesha nchi kisasa. Msome hapa uone anafanyaje kazi zake?
Comments
Post a Comment