MAKALA BAYERN MUNICH Vs BORUSSIA DORTMUND FAINALI YA KIHISTORIA
Wakati tunaelekea kuangalia nini kitatokea fainali kati ya hawa mabingwa wawili tusome kidogo makala hii kujua historia zao.
FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 25
kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England haitakuwa ya Wajerumani tu,
badala yake yenye ufundi mwingi zaidi.
Takwimu za Ligi ya Mabingwa Ulaya tokea
ilipoanza msimu huu, zinaonyesha Bayern Munich ndiyo timu bora hadi sasa na
Borussia Dortmund inafuatia.
Takwimu za ubora za ligi ya mabingwa
zimeonyesha hazikuwa na kasoro, kwani timu zilioonekana bora kihesabu ndizo
zilizongia fainali.
Swali linakuja hivi, Bayern Munich inayoonekana
ni bora zaidi kwa mujibu wa takwimu, ndiyo itakayobeba ubingwa?
Kuna mengi ya kujiuliza na kujadili,
kwani takwimu hupewa asilimia 50 kwa kuwa mchezo wa soka una mabadiliko. Lakini
safari hii zimeonyesha zina nguvu ndiyo maana timu mbili bora kitakwimu
zimaingia fainali.
Bado inaonekana Bayern ni bingwa kwa
takwimu, lakini Dortmund inaonekana si timu ya mzaha na hatari zaidi mechi hiyo
ina ukubwa maradufu, maana itakuwa ni mechi ya watani wa jadi na wapinzani
wakubwa ambao watakuwa wanacheza ugenini.
Mechi za wapinzani wakubwa mara nyingi
huwa hazitabiriki, hata timu iliyo bora zaidi kitakwimu inaweza kuangushwa.
Lazima Bayern wanalijua hilo na watalifanyia kazi.
Bundesliga:
Achana na kwamba tayari Bayern ni
mabingwa wapya wa Bundesliga, lakini katika mechi nane za timu hizo katika ligi
hiyo zinaonyesha kweli ziko imara.
Bayern imeshinda mechi zake zote nane
zilizopita, Dortmund imepoteza mechi moja katika hizo, maana yake imeshinda
saba.
Timu zote mbili ni bora katika
ushambuliaji na ulinzi, lakini zinacheza kwa nguvu na zimeonyesha katika mechi
zao kuwa wachezaji wengi wana nguvu.
Katika mechi kati ya Bayern na
Barcelona, Wajerumani hao walionekana kuwazidi pumzi na nguvu Barca. Ilikuwa
utafikiri timu ya ligi kuu na ile ya daraja la kwanza.
Lakini Dortmund walipocheza na Real
Madrid, hasa mechi ya pili mjini Madrid. Pamoja na kufungwa, Wajerumani hao
walionekana ni bora zaidi ya vijana wa Jose Mourinho katika stamina.
Madrid ni kati ya timu zenye ubora wa
juu katika stamina, wanapoonekana wako katika wakati mgumu dhidi ya timu fulani
katika kiwango cha stamina, maana yake lazima timu hiyo ingaliwe kwa jicho la
tatu.
Mechi hizo za nusu fainali ndiyo
zimeamsha mambo mengi sana, mfano hilo la stamina, pumzi na hata ufundi.
Lakini timu hizo zimecheza kwa kiwango
cha juu tokea kuanza kwa mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kila timu iliongoza kundi lake, baada ya
hapo zikaendelea kushinda karibu kila mechi lakini Dortmund hadi imetinga nusu
fainali, ilikuwa haijapoteza hata mechi moja hadi ilipofungwa na Madrid mabao
2-0, lakini ikaingia fainali.
Ujerumani:
Ukiangalia kwa michuano yote ya
Ujerumani mwaka jana na huu, timu hizo zimekutana mara tano katika Super Cup,
Bundesliga na Kombe la Shirikisho la Soka la Ujerumani maarufu kama DFB Polka.
Katika mechi hizo, Bayern imeshinda
mechi mechi tatu, Dortmund imeshinda moja kwa mabao 5-2 na sare ni moja. Hii ni
picha kwamba bado Munich inabebwa na takwimu, lakini Dortmund inaweza kugeuza
mchezo na kushinda kwa kuwa imewahi kufanya hivyo.
Mabao:
Kila timu ina uwezo wa aina yake wa
kupachika mabao, inaonyesha kama kuna hali fulani ya kufanana katika ufungaji
wa mabao hasa katika mechi za ligi ya mabingwa walizocheza.
Asilimia 41.4 ya mabao ya Bayern
yamefungwa katika kipindi cha kwanza katika Ligi ya Mabingwa na kipindi cha
pili, mabao yaliyofungwa ni 58.6%.
Dortimund wamefunga mabao yao katika
kipindi cha kwanza kwa asilimia 42.3 wakati kipindi cha pili ni 57.7%.
Maana yake kila timu ina uwezo wa
kufunga mabao zaidi katika kipindi cha pili
Hakika haitakuwa mechi laini kwa kuwa
timu hizo mbili zinajuana vizuri. Angalia Dortmund iliibuka na kutawala misimu
miwili iliyopita.
Lakini Bayern wakabadili gia na mambo
yakawa tofauti msimu huu na kufanikiwa kutwaa ubingwa mapema wakiwa na mechi
tano mkononi, maana yake walijua walipoteleza.
Wanaweza kuendeleza ubora wao huo,
lakini inawezekana kabisa hata Dortmund wakawa wamejiuliza na kujua wapi
waliteleza, wakafanya makubwa.
Kama itabaki suala la kuamini ubora wa
takwimu, basi inaonyesha Dortmund itabaki nafasi ya pili, Munich itakuwa
bingwa.
MECHI ZAO ZA MWISHO UJERUMANI:
Feb 27,2013 German Cup Bayern
1 - 0 Dortmund
Des 12,2012 BundesLiga
Bayern 1 - 1 Dortmund
Agst 12,2012 Super Cup Bayern
2 - 1 Dortmund
Mei 12,1212 German Cup
Dortmund 5 - 2 Bayern
Apr 11,2012 BundesLiga
Dortmund 1 - 0 Bayern
ZIMEKUTANA MARA NGAPI?
Shinda Poteza Sare
Kombe la DFB (Dortmund ) 1 2
0
DFB Pokal (Bayern )
2 1 0
Kombe la DFB (Dortmund) 7 8 5
Bundesliga (Bayern) 8 7 5
Super Cup (Dortmund ) 1 1 0
Super Cup (Bayern)
1 1 0
UBORA LIGI YA MABINGWA
P W D
L GF
GA Dif
Pts
1 Bayern Munich 12
9 1
2 29
10 +19
28
2 Dortmund
12 4 1 23
12 +11
25 3 Paris SG
10 6
3 1
20 8
+12 21
4 Real Madrid 12 6 3 3 26
18 +8
21
5 Juventus
10 5 3 2 17
8 +9
18 6 FC Barcelona
12 5 3 4 18
17 +1
18
FIN.
Tusubiri kushuhudia nini kitatokea...
Comments
Post a Comment