SHEREHE LAFANYIKA JIJINI MANCHESTER KUMUAGA SIR ALEX FERGIE
Mabingwa
wa ligi kuu soka nchini Uingereza, Manchester United
leo hii wamepiga bonge la sherehe kushangilia ubingwa wao wa 20 pamoja
na kumuaga rasmi kocha wao aliyewafundisha kwa miaka 27 na kutwaa
makombe 49 katika michuano mbalimbali.
Viongozi,
wachezaji na mashabiki wa United leo hii wamepita mitaa mbalimbali ya
jijini Manchester kushangilia ubingwa wao na kumuaga Ferguson kwa
heshima kubwa.
Kocha
Kibabu leo hii kaagwa rasmi na kubwaga manyanga ya kuwanoa United na
kazi yake kumrithisha kocha ambaye amemhusudu kwa muda mrefu, David
Moyes ambaye kwa sasa ni kocha wa Everton.
Ferguson
amesitaafu huku akiwa tayari amesharejesha ubingwa alionyang`anywa na
watani zake wa jadi Manchester City msimu uliopita na kupeleka adhaa
kubwa kwa kocha wa City, Roberto Mancini ambaye kibarua chake kinaweza
kuinga mchanga wakati wowote baada ya kufanya vibaya msimu huu.
Feguson amekaa na timu kwa miaka 27, ni ngumu kujua kama Moyes ataweza kukaa muda kama wake akiwa na United ama la.
Watu wengi walidhani Mreno Jose Mourinho angebeba mikoba ya Fergie lakini imekuwa taofauti kabisa.
Ndani ya Albert Square
Comments
Post a Comment