MAKALA BAYERN MUNICH Vs BORUSSIA DORTMUND FAINALI YA KIHISTORIA



Wakati tunaelekea kuangalia nini kitatokea fainali kati ya hawa mabingwa wawili tusome kidogo makala hii kujua historia zao.
FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England haitakuwa ya Wajerumani tu, badala yake yenye ufundi mwingi zaidi.
Takwimu za Ligi ya Mabingwa Ulaya tokea ilipoanza msimu huu, zinaonyesha Bayern Munich ndiyo timu bora hadi sasa na Borussia Dortmund inafuatia.
Takwimu za ubora za ligi ya mabingwa zimeonyesha hazikuwa na kasoro, kwani timu zilioonekana bora kihesabu ndizo zilizongia fainali.
Swali linakuja hivi, Bayern Munich inayoonekana ni bora zaidi kwa mujibu wa takwimu, ndiyo itakayobeba ubingwa? 
Kuna mengi ya kujiuliza na kujadili, kwani takwimu hupewa asilimia 50 kwa kuwa mchezo wa soka una mabadiliko. Lakini safari hii zimeonyesha zina nguvu ndiyo maana timu mbili bora kitakwimu zimaingia fainali.
Bado inaonekana Bayern ni bingwa kwa takwimu, lakini Dortmund inaonekana si timu ya mzaha na hatari zaidi mechi hiyo ina ukubwa maradufu, maana itakuwa ni mechi ya watani wa jadi na wapinzani wakubwa ambao watakuwa wanacheza ugenini.

Mechi za wapinzani wakubwa mara nyingi huwa hazitabiriki, hata timu iliyo bora zaidi kitakwimu inaweza kuangushwa. Lazima Bayern wanalijua hilo na watalifanyia kazi.
Bundesliga:
Achana na kwamba tayari Bayern ni mabingwa wapya wa Bundesliga, lakini katika mechi nane za timu hizo katika ligi hiyo zinaonyesha kweli ziko imara.

Bayern imeshinda mechi zake zote nane zilizopita, Dortmund imepoteza mechi moja katika hizo, maana yake imeshinda saba.
Timu zote mbili ni bora katika ushambuliaji na ulinzi, lakini zinacheza kwa nguvu na zimeonyesha katika mechi zao kuwa wachezaji wengi wana nguvu.
Katika mechi kati ya Bayern na Barcelona, Wajerumani hao walionekana kuwazidi pumzi na nguvu Barca. Ilikuwa utafikiri timu ya ligi kuu na ile ya daraja la kwanza.
Lakini Dortmund walipocheza na Real Madrid, hasa mechi ya pili mjini Madrid. Pamoja na kufungwa, Wajerumani hao walionekana ni bora zaidi ya vijana wa Jose Mourinho katika stamina.
Madrid ni kati ya timu zenye ubora wa juu katika stamina, wanapoonekana wako katika wakati mgumu dhidi ya timu fulani katika kiwango cha stamina, maana yake lazima timu hiyo ingaliwe kwa jicho la tatu.
Mechi hizo za nusu fainali ndiyo zimeamsha mambo mengi sana, mfano hilo la stamina, pumzi na hata ufundi. 
Lakini timu hizo zimecheza kwa kiwango cha juu tokea kuanza kwa mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kila timu iliongoza kundi lake, baada ya hapo zikaendelea kushinda karibu kila mechi lakini Dortmund hadi imetinga nusu fainali, ilikuwa haijapoteza hata mechi moja hadi ilipofungwa na Madrid mabao 2-0, lakini ikaingia fainali.
Ujerumani:
Ukiangalia kwa michuano yote ya Ujerumani mwaka jana na huu, timu hizo zimekutana mara tano katika Super Cup, Bundesliga na Kombe la Shirikisho la Soka la Ujerumani maarufu kama DFB Polka.
Katika mechi hizo, Bayern imeshinda mechi mechi tatu, Dortmund imeshinda moja kwa mabao 5-2 na sare ni moja. Hii ni picha kwamba bado Munich inabebwa na takwimu, lakini Dortmund inaweza kugeuza mchezo na kushinda kwa kuwa imewahi kufanya hivyo.
Mabao:
Kila timu ina uwezo wa aina yake wa kupachika mabao, inaonyesha kama kuna hali fulani ya kufanana katika ufungaji wa mabao hasa katika mechi za ligi ya mabingwa walizocheza.
Asilimia 41.4 ya mabao ya Bayern yamefungwa katika kipindi cha kwanza katika Ligi ya Mabingwa na kipindi cha pili, mabao yaliyofungwa ni 58.6%.
Dortimund wamefunga mabao yao katika kipindi cha kwanza kwa asilimia 42.3 wakati kipindi cha pili ni 57.7%.
Maana yake kila timu ina uwezo wa kufunga mabao zaidi katika kipindi cha pili
Hakika haitakuwa mechi laini kwa kuwa timu hizo mbili zinajuana vizuri. Angalia Dortmund iliibuka na kutawala misimu miwili iliyopita.
Lakini Bayern wakabadili gia na mambo yakawa tofauti msimu huu na kufanikiwa kutwaa ubingwa mapema wakiwa na mechi tano mkononi, maana yake walijua walipoteleza.
Wanaweza kuendeleza ubora wao huo, lakini inawezekana kabisa hata Dortmund wakawa wamejiuliza na kujua wapi waliteleza, wakafanya makubwa.
Kama itabaki suala la kuamini ubora wa takwimu, basi inaonyesha Dortmund itabaki nafasi ya pili, Munich itakuwa bingwa.
MECHI ZAO ZA MWISHO UJERUMANI:
Feb 27,2013       German Cup       Bayern 1 - 0       Dortmund
Des 12,2012       BundesLiga         Bayern 1 - 1       Dortmund
Agst 12,2012      Super Cup            Bayern 2 - 1        Dortmund
Mei 12,1212       German Cup       Dortmund 5 - 2  Bayern
Apr 11,2012        BundesLiga         Dortmund 1 - 0  Bayern 

ZIMEKUTANA MARA NGAPI?
                                                               Shinda Poteza       Sare
          Kombe la DFB (Dortmund )           1            2              0
          DFB Pokal (Bayern )                       2            1             0
            Kombe la DFB (Dortmund)          7            8             5
              Bundesliga (Bayern)                   8             7             5
          Super Cup (Dortmund )                 1             1             0
          Super Cup (Bayern)                       1             1             0
           
UBORA LIGI YA MABINGWA
                                                P        W      D       L        GF     GA     Dif     Pts   
1          Bayern Munich          12     9       1        2       29       10      +19     28    
2          Dortmund                    12            4       1       23     12     +11   25   3          Paris SG                              10    6       3       1       20     8       +12   21    4          Real Madrid                       12    6       3       3       26     18     +8     21    
5          Juventus                     10    5       3       2       17     8       +9     18              6          FC Barcelona            12      5       3       4       18     17     +1     18    















FIN.
 
Tusubiri kushuhudia nini kitatokea...

Comments