MELI YA MV SEAGUL YAZAMA



Meli hiyo ya abilia na mizigo ilikuwa na abiria wapatao 200 imezama eneo la Chumbe na juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari baadhi ya watu wameokolewa wakiwa hai na wengine bado wanaelea wakiwa na maboya. Taarifa za vifo bado hazijathibitishwa japo ukweli ni kwamba vifo vinatajwa kutokea.

Mara kadhaa meli hiyo imewahi kuripotiwa kuwa mbovu, huku ikiendelea kutoa huduma licha ya taarifa hizo.
Waokozi wako kwa wingi eneo la tukio wakijaribu kuinasua miili iliyozama....
Kamishna wa jeshi la polisi mjini Zanzibar, Musa Ally Mussa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Comments